LEO KATIKA MICHEZO.

Samwel Eto’o afuta kesi ya Barcelona




Mchezaji wa zamani wa Barcelona Samweli Eto’o amefuta kesi madai aliyokuwa amefungua akiidai timu hiyo euro milioni tatu.
Eto’o alikuwa anaidai timu hiyo kutokana na uhamisho wake kutoka Barcelona kwenda Inter Milan mwaka 2010.

Klabu ya Barcelona imesemakuwa imepokea barua kutoka katika mahakama iliyokua ikisikiliza kesi hiyo ikieleza uamuzi huo Eto’o.
Katika kesi hiyo Eto’o alikuwa akidai fidia ya kiasi kingine cha fedha kisichojulikana kutokana na uhamisho huo.
Awali Klabu ya Barcelona iliilipa Inter Milan kitita cha dola za kimarekani milioni 66 kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji Milan Zlatan Ibrahimovic fedha ambazo zilijumuisha pia uhamisho wa Eto’o kutoka Barcelona kwenda Inter Milan.
Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Cameroon alikua ni miongoni mwa wachezaji walioleta mafanikio katika klabu ya Barcelona akiifungia magoli 152 kabla hajahamia Inter Milan.
Hata hivyo Eto’o aliihama Inter Milan mwaka uliopita alihamia katika klabu ya Anzhi Makhackala ya Urusi.


 

Bayer Leverkusen yamtimua kocha Robin Dutt.


  Bayer Leverkusen ilimmwonyesha mlango kocha wake Robin Dutt baada ya timu yake kushindwa magoli mawili kwa sifuri na Freiburg huku beki wa zamani wa Liverpool Sammi Hyypia akiteuliwa kuwa kaimu Mkufunzi.
 
Dutt alifika mbele ya Mkurugenzi wa Spoti wa Leverkusen Rudi Voeller na Mwenyekiti Wolgang Holzhaeser Jana Jumapili asubuhi ambapo alipigwa kalamu rasmi. Katika kipindi kilichosalia cha msimu na michuano sita ijayo, beki wa zamani wa Leverkusen na Liverpool raia wa Finland Hyypia atakuwa kocha pamoja na mkufunzi wa kikosi cha Leverkusen cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19.Bayer ni mojawapo ya timu nne ambazo zina pointi 40 na ni sharti zimalize miongoni mwa timu saba za kwanza ili kujihakikishia nafasi ya kucheza katika Europa League, baada ya timu hiyo kufikia awamu ya 16 ya ligi ya Mabingwa Ulaya. Dutt ni kocha wa nane kufurushwa na klabu ya Bundesliga msimu huu. Anafuata Marcus Sorg (Freiburg), Michael Oenning (Hamburg), Holger Stanislawski (Hoffenheim) na Marco Kurz (Kaiserslautern), huku nayo Hertha Berlin ikawapiga kalamu Markus Babbel na kisha Michael Skibbe msimu huu.

No comments:

Post a Comment