HISTORIA FUPI YA MAREHEMU KANUMBA.

                    Steven Charles Kanumba (8 Januari 1984, Shinyanga – 7 Aprili, 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa wa Kinigeria nchini.

Steven Kanumba
Steven-Kanumba.jpg






Steven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya “90″. Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.
Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to Lagos, She is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.
                         Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
 
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
 
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

Filamu na Tamthilia Alizotunga. 

1 Tufani ( Johari )
2 Gharika
3 Baragumu
4 Sikitiko Langu
5 Johari 2
6 Dangerous Desire
7 Dar 2 Lagos
8 Cross my Sin
9 Village Pastor
10 Family Tears Filamu na Tamthilia Alizoigiza 1 Jahazi ( Tamthilia )
2 Dira ( Tamthilia )
3 Tufani ( Johari )
4 Gharika( Tamthilia )
5 Baragumu( Tamthilia )
6 Sikitiko Langu ( Filamu )
7 Johari 2 ( Filamu )
8 Dangerous Desire ( Filamu )
9 Dar 2 Lagosi
10 Riziki ( Filamu ) 11 Cross my Sin( Filamu )
12 Uncle JJ (Filamu)
Na nyinginezo nyingi sana……
Steven Kanumba alitangaza hivi karibuni nia ya kuwa mgombea wa ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi. Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasnia ya filamu Tanzania na Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.

Mwenyezi mungu akuweke pema na penye nuru…..Amen.!

No comments:

Post a Comment