WEMA AAMUA KUJIBU MAPIGO BAADA YA DIAMOND KUSEMA KUWA
WEMA ALIYATAKA MWENYEWE,
Baada kumdhalilisha Wema Isaac
Sepetu mwishoni mwa wiki iliyopita, ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul
‘Diamond’ amesema kuwa mpenzi wake huyo wa zamani alijitakia mwenyewe.
Akizungumza na Kashaiblog
katika mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa, Wema alishindwa kusoma alama za
nyakati kwani hakupaswa kunyanyuka kwenda kumtunza lakini kwa kuwa hakulifahamu
hilo, ndiyo maana yakamkuta yaliyomkuta.
“Siwezi kumuomba radhi Wema,”
alisema Diamond na alipoulizwa kwa nini asifanye hivyo akajibu:
“Aliyataka mwenyewe, siku hiyo mchana kuna vitu vilitokea na kabla sijaenda ukumbini so kama Wema angevikumbuka asingethubutu kufanya vile.”
“Aliyataka mwenyewe, siku hiyo mchana kuna vitu vilitokea na kabla sijaenda ukumbini so kama Wema angevikumbuka asingethubutu kufanya vile.”
Diamond anayewania Tuzo za Kili 2012 akiwa kwenye ‘kategori’ sita, alisema kuwa ishu haikuanzia pale ukumbini kwani Wema alimfuata mazoezini mchana wa siku hiyo, lakini hakuonana naye.
Alisema: “Nilipoamka asubuhi
nilijiandaa na kwenda mazoezini, ghafla nilipigiwa simu na mtu nikaenda mahali,
kabla sijafika huko nilipigiwa simu kuwa Wema amenifuata mazoezini, nilishangaa
hivi huyu mwanamke vipi?
“Nikamwambia aliyenipigia simu kuwa sirudi hadi aondoke na kweli sikurudi hadi Wema alipoondoka.”
“Nikamwambia aliyenipigia simu kuwa sirudi hadi aondoke na kweli sikurudi hadi Wema alipoondoka.”
Diamond aliendelea kutambaa na mistari kuwa baada ya jaribio lake la kumfuata ukumbini kushindikana, Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, alitinga nyumbani kwake usiku akiwa ameongozana na rafiki yake wa kiume aliyemtaja kwa jina la Rommy.
“Nilimpigia simu Rommy aje nyumbani
kuchukua tiketi ya kuingia kwenye shoo, nilishangaa aliponiambia kuwa Wema
alimng’ng’ania na kuja naye nyumbani kwangu eti kuniomba msamaha, kiukweli
alinivuruga hadi nikachelewa kwenye shoo.
“Nilikurupuka kwa hasira kwenda sebuleni kutaka kumpiga, namshukuru Mungu, mama na mjomba wangu walinizuia, mwisho wake mjomba akaamua kwenda kumwambia Wema aondoke,” alisema staa huyo wa kibao cha Moyo Wangu.
WEMA
AJIBU MAPIGO
Baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Diamond, Kashaiblog Tulizungumza na Wema ambaye naye alijibu mapigo na kusema Diamond ni mswahili.
Baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Diamond, Kashaiblog Tulizungumza na Wema ambaye naye alijibu mapigo na kusema Diamond ni mswahili.
“Sikutegemea kama Diamond angekuwa
mswahili kiasi kile, hadi kushindwa kuchukua fedha ambazo nilikuwa namtunza.
“Nilikwenda ukumbini baada ya meneja
wangu, Martin Kadinda kuniomba nikamuache pale.
Pia nilikwenda nyumbani kwa akina Diamond baada ya Rommy kuniomba nimpeleke akachukue tiketi yake.
Pia nilikwenda nyumbani kwa akina Diamond baada ya Rommy kuniomba nimpeleke akachukue tiketi yake.
“Nilipofika nyumbani kwao nilimuona
mama yake Diamond akiwa nje, nikaenda kumsalimia, ghafla Rommy aliyekuwa
ameingia ndani alitoka tukaondoka.”
Katika kuonyesha kuwa fedha si kitu
kwake siku ya shoo, Wema alinunua meza kwa ajili ya kukaa na mastaa wenzake.
“Siku ile nilikwenda kwa ajili ya
kubadilishana mawazo na marafiki zangu ndiyo maana nikanunua meza kwa ajili ya
kukaa na mastaa wenzangu kama Ray (Vincent Kigosi), Wolper (Jacqueline) JB
(Jacob Steven) na wengine lakini kwa bahati mbaya hawakutokea,” alisema Wema na
kuongeza:
“Kilichotokea pale ukumbini ni
kwamba nilikwenda kutunza kama nilivyowatunza wengine. Labda kujichetua
kwangu ndiko kulikoniponza, unajua kuachana na mtu si kuwekeana bifu, ni jambo
la kawaida.”
Kama unakumbuka Mwishoni mwa wiki
iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar, kulifanyika shoo kubwa ya
Diamond iliyokwenda kwa jina la Diamonds Are Forever ambapo Wema alikwenda
kumtunza msanii huyo lakini jamaa akakataa kupokea fedha ya mrembo huyo.
No comments:
Post a Comment