Kesi ya vurugu wakati wa mechi za timu za Al- Masry na Al- Ahly kusikilizwa April 17




Kesi ya vurugu wakati wa mechi za timu za Al- Masry na Al- Ahly kusikilizwa April 17
Watu 75 wanataraji kusimama kizimbani tarehe 17 mwezi April ,kujibu tuhuma kuhusiana na tuhuma za vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wa soka katika mji wa Port Said nchini Misri miezi miwili iliyopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70.
Shirika la habari la taifa hilo MENA limetoa taarifa hiyo na kwamba askari polisi tisa ni miongoni mwa watakao simama upande wa utetezi katika kesi hiyo ambayo itasikilizwa mjini Cairo kwa sababu za kiusalama.
Februari mosi mwaka huu, katika mji wa Port Said ,kulitokea vurugu baina ya mashabiki wa timu za Al- Masry na Al- Ahly kufuatia timu ya Al- Masry iliyokuwa ikicheza nyumbani kuwavamia na kuwashambulia kwa mawe na chupa mashabiki wa timu ya Al – Ahly baada ya timu yao kufungwa magoli 3-1.

No comments:

Post a Comment