Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic afungiwa mechi tatu.

 
Mlinzi wa klabu ya Chelsea Branislav Ivanovic amefungiwa kucheza mechi tatu baada ya kupatikana na hatia ya kufanya vurugu katika mchezo walioshinda dhidi ya Wigan siku ya Jumamosi.

Chama cha Kandanda cha England (FA) kilimtia hatiani mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia siku ya Jumanne baada ya picha za mkanda wa video kuonesha akimtandika ngumi Shaun Maloney kabla Juan Mata hajapachika bao la ushindi.

Ivanovic alipinga mashtaka hayo lakini jopo la wajumbe wa FA likashikilia alikuwa na hatia.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 atakosa michezo mitatu ijayo ya Chelsea, ukiwemo ule wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham.
FA waliweza kuchukua hatua hiyo kwa kufuata utaratibu wa makosa yaliyopita kwa sababu mwamuzi Mike Jones na wasaidizi wake hawakuona tukio likitendeka wakati huo.
Pamoja na mechi dhidi ya Tottenham, Ivanovic hataweza kuitetea Chelsea wakati itakapokwenda kucheza dhidi ya Arsenal tarehe 21 mwezi huu wa Aprili na pia siku nane baadae dhidi ya QPR.

No comments:

Post a Comment