Habari za kusikitisha Rais wa Malawi Bingu wa amefariki dunia
baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo, akiwa na miaka 78. Habari kutoka kwa
serikali zimethibitisha kifo hicho kwa BBC.
Mwili wa wa kiongozi huyo
umepelekwa Afrika Kusini.
Hata hivyo serikali haijatoa taarifa rasmi
kuhusu kifo cha Wa-Mutharika. Mmoja wa madaktari waliokuwa wakimhudumia
kiongozi huyo ameambia BBC, Wa-Mutharika alikufa baada ya moyo wake
kusimama.
Wadadisi wameonya kifo cha rais huyo
huenda kikazua mgogoro wa uwongozi. Katiba ya nchi inampa nafasi Makamu
wa Rais kuongoza nchi endapo Rais atafariki au kuugua kiasi cha
kushindwa kuongoza taifa.Hata hivyo Makamu wa Rais nchini Malawi, Joyce
Banda alitofautiana na Wa-Mutharika kufuatia mzozo wa urithi wa uongozi
ambapo alifukuzwa kutoka chama tawala, Democratic People's Party (DPP).
Bingu wa Mutharika aliingia madarakani
mwaka wa 2004. Alikihama chama chake cha United Democratic Front
(UDF) kwa tuhuma za wanachama kuhujumu harakati za kupambana na
ufisadi. Alichaguliwa tena mwaka 2009, lakini katika siku za karibuni
wakosoaji wake wamemlaumu kwa kuegemea sera za kiimla.
Rais huyo alikumbwa na shinikizo za
kuachia madaraka kwa tuhuma za kupendelea ukoo wake, na kuharibu
madaraka.Wa Mutharika aliwakera wafadhili wa kigeni hasa baada ya
kumfukuza balozi wa Uingereza Fergus Cochrane-Dyet, na kufanya utawala
wa Uingereza kusimamisha msaada kwa nchi hiyo ya Malawi.
No comments:
Post a Comment