ELIZABETH MICHAEL (LULU) AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO, HUKU KESI YAKE IKIPANGWA KUSOMWA TENA APRIL 23, 2012



 
 
 
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Bi. Elizabeth Michael leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka yake ya kuhusu  kifo cha muigizaji mwenzake  nchini Marehemu Steven Kanumba. 

Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini, Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.

Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565. 

Habari kwa Hisani  Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment