KANUMBA AFARIKIA DUNIAAAAA USIKU WA KUAMKIA LEO.
Habari
zilizonifikia hivi sasa zinasema msanii maarufu nchini, Steven Kanumba
amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo
akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo
limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka
kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye
kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini
alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa
sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
hospitali ya Taifa Muhimbili
Inaendelea....
Taarifa nilizozipata sasa hivi ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA
amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka
na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo
wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli
kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa
Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na
Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya
kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka
nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake
wamefuka pamoja na watu mbalimbali, kashaiblog itaendelea
kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.
Ila kumekua na taarifa nyingine
ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani
baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na
kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati
akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka
alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo
alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili
ambako muda mfupi baadae alifariki dunia,
Msanii Johari akiwa na majonzi makubwa |
![]() |
Wema sepetu huzun ukiwa umemtawala hajui afanye nin. |
Picha za kanumba enzi za uhai wake.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEM PEMA PEPONI
AMEN!!!!!!
No comments:
Post a Comment