MAWAZIRI WAPYA WASEMA HIVI!!!!

Mawaziri walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete , wametoa kauli zenye kuleta matumaini mapya, huku wakielezea changamoto zinazowakabili katika kazi hiyo muhimu ya kitaifa.Baadhi ya mawaziri wapya na naibu mawaziri, wakizigusia changamoto zinazozikabili wizara zao na namna ya kuondokana nazo.
Hata hivyo, mawaziri na naibu mawaziri wengine hawakuwa tayari kuzungumza na gazeti hili, badala yake waliahidi kutoa tamko rasmi baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam kesho.

Waziri mteule wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, alisema mara baada ya kuapishwa , anatarajia kuanza kazi kwa kukishughulikia kilio cha muda mrefu cha madaktari kwa kusikiliza ripoti ya kamati maalum iliyoundwa.
“Ipo kamati iliyohusisha wajumbe kutoka serikalini na madaktari ambayo ilikuwa ikiangalia changamoto zilizotolewa na madaktari wakati wa mgomo. Nitaisikiliza imekuja na maoni gani kisha kazi ianze,” aliahidi.
Aliongeza kuwa, kasi ya kuyatatua matatizo hayo itategemeana na uwezo wa bajeti ya serikali.
Suala jingine aliloahidi kulipa kipaumbele ni pamoja na Bohari ya Dawa (MSD) ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wadau wengi juu ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba usioridhisha .
“Kwenye hili tutaangalia upya utaratibu wa kusambaza dawa ili maeneo yote yaweze kufikiwa kwa muda na wakati, lakini pia mfuko wa Bima ya Afya nao tutauangalia kwa mapana yake ili uweze kukidhi matakwa ya wanachama wake wote,” alisema.

Naibu Waziri mteule wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, kwa upande wake alisema moja ya kazi watakayoanza nayo ni kuangalia gharama za simu za mitandao ambazo zimekuwa zikiwaumiza watumiaji.
“Mteja anaweka vocha ya Sh. 2,000 kwenye simu yake anaongea kidogo tu fedha yote inaliwa, kwa kweli hili lazima tulitazame maana wanasema gharama zao wamezipunguza lakini mtumiaji anaumia,” alisema.
 wanatarajia kupanua zaidi mkonga wa Mawasiliano wa Taifa ili maeneo mengi nchini yaweze kufikiwa na huduma za mawasiliano.
Pia Makamba alisema wizara yake inatarajia kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na wataalamu wengi wa sayansi badala ya kutegemea watu wageni kutoka nje.
“Hapa tutakachofanya ni kuwafanya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi kama masomo mengine, ili nchi iendelee lazima izalishe wanasayansi wapya wazalendo na msingi wa maendeleo ni sayansi inayotakiwa kuanzia ngazi ya chini,” alisema.
Kwa upande wa Kampuni ya Simu Nchini TTCL , Makamba alisema wanatarajia kuipa hadhi na heshima TTCL, kwa kuziangalia changamoto zake ambazo zinaifanya ibaki nyuma ya kampuni nyingine za simu.
Akizungumzia masuala ya kukwamishwa na bajeti Makamba alisema kikubwa ni wizara kutengeneza hoja za kuitetea kama ilivyofanya Wizara ya Ujenzi mwaka jana ambapo Waziri wake aliweza kupata bajeti ya Sh. Trilioni 1.4 baada ya kujitetea kwa hoja madhubuti.

Dk. H Mwakyembe ambaye awali alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na kuteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi alisema kwa kifupi kuwa, kwa sasa hawezi kuzungumza lolote mpaka atakapoapishwa.
“Najua unatamani kujua mikakati ya wizara yangu mpya niliyopelekwa lakini ndugu mwandishi nitafanya hivyo mara baada ya kuapishwa,” alisema na kukata simu.

Waziri mteule wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kaghasheki, alisema hawezi kuzungumza na mwandishi kwenye simu na kwamba yeyote anayetaka kumhoji amfuate ofisini.
“Kwanza sijaapishwa na pia siku hizi kuna wajanja wengi, wanajitambulisha kwenye simu kuwa ni waandishi kumbe sio, tafadhali njoo ofisini kwangu tutaongea,” alishauri.

Waziri mteule wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, alisema baada ya kuteuliwa anasubiri kuapishwa ili kuanza kazi rasmi.
Wadau wengine waliozungumzia Baraza Jipya la Mawaziri ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, ambaye kupitia mtandao wake, alisema juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katika utumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda.
Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alimpongeza George Mkuchika , kwa kuwa mtulivu asiyekuwa na makuu wala kujitetea kama mawaziri watuhumiwa wengine.
Mkuchika amemrudisha kwenye baraza jipya kuwa Waziri wa Utawala Bora.
Aliwaonya mawaziri wateule juu ya kusherehekea uteuzi wao “Kwa kawaida wateule hufanya sherehe, nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia, nitawashangaa watakaoenda kuapa kwa maua kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu” ilisema sehemu ya safu hiyo na kuongeza:
“Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na wateule wote watakuwa kikaangoni, Too short honeymoon, hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi inachangamoto nyingi” iliongeza.
Aliwaambia kuwa kazi iliyopo ni kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwa wananchi wengi, kukuza uchumi wa vijiji na uzalishaji viwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana. alitoa changamoto nyingine kuwa ni pamoja na kuongeza mapato ya utalii kutoka katika hifadhi za taifa na kuvutia watalii.
“Nimewapigia simu wateule wengi na kuwaambia siwapi pongezi bali nawatakia kazi njema na uwajibikaji kwa sababu ndio msingi wa kupambana na rushwa, uvivu na uzembe,” ilisema safu yake.
Kabwe ambaye ni Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi katika mtandao wake alimwambia Waziri mteule wa wizara hiyo, Dk. William Mgimwa, kuwa uteuzi wake ni changamoto kubwa katika maisha yake.
“Eneo lenye bajeti kubwa kuliko zote ni huduma kwa deni la taifa lazima kuangalia upya deni hili, kwa sasa ukilijumlisha na dhamana za serikali limefikia Shilingi tilioni 22 hadi Desemba mwaka 2011,” alisema na kuongeza:
“Nimewahi kutaka ukaguzi maalum katika ‘account’ ya deni la taifa. Ninarejea wigo huu, tunalipa takriban Shilingi tilioni 1.9 kwa mwaka ambayo ni zaidi ya bajeti ya miundombinu, afya, maji na umeme.”
Alimkumbusha Dk. Mwakyembe kuwa atakumbukwa iwapo ataimarisha na kuufanya usafiri wa reli ufanye kazi.
Aidha, alisema nchi inatumia Shilingi bilioni 300 kwa mwaka kukarabati barabara wakati inahitaji Shilingi bilioni 200 kukarabati reli kusafirisha mizigo kwenda na kutoka bandarini.

YALIYOJIRI KWENYE KILI MUSIC AWARD WINNERS MWANZA

 Show ya hapa Mwanza ilifunguliwa na msanii wa taarabu Isha Mashauzi,
 Akafuatia msanii aliyechukuwa tuzo ya RnB anajulikana kama Ben Pol
 Misago, Hellen & Dullah
Barnaba, Hellen & Sam Misago
Kaka mkubwa ndio aliyekuwa akiangalia ulinzi wa wasanii wote wakiwa salama
Ommy Dimpoz akiwa stejini.
 Barnaba
 DD   A.K.A    Diamond Dancers
AT akiwakatisha mauno.
 Diamond akiwalaza salama.
ROMA akifunga Show.

WATANZANIA TUMCHANGIE SAJUKI AKATIBIWE.

RAIS ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.
Rais Jakaya Kikwete hivi punde ametangaza Baraza jipya la Mawaziri likiwa na sura mpya wakati baadhi ya Mawaziri wakibaki katika nafasi zao. Ifuatayo ni orodha ya Mawaziri hao walioteuliwa pamoja na Manaibu Waziri.…

 Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. William Ngeleja.
 Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Ezekiel Maige.…

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkulo.
 Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Ezekiel Maige.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dr Cyril Chami.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.
Wanahabari wakiwajibika wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.…

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.
Wanahabari wakiwajibika wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri leo Aprili 4, 2012.

 ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
MAWAZIRI
1.  OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2.         
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3.            
OFISI  YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4.          
  WIZARA 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika MasharikiNdugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa UjenziDr.  John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya UfundiDr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na WatotoNdugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa KimataifaNdugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya NchiNdugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na UvuviDr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na TeknolojiaProf.  Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe,  Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara MaalumProf. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa  Kilimo, Chakula na UshirikaEng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na MichezoDr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na MadiniProf. Sospeter Muhongo, Mb.,

5.          
NAIBU MAWAZIRI  OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI

6.
           OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa RaisNdugu Charles Kitwanga, Mb.,

7.            OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8.          WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na AjiraDr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na UshirikaNdugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya NchiNdugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na BiasharaNdugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na UvuviNdugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa KimataifaNdugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi,Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na UtaliiNdugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa UjenziNdugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na MadiniNdugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa UchukuziDr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na MichezoNdugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na SheriaNdugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa FedhaNdugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa FedhaNdugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012

KANUMBA ACHUKULIWA MSUKULE

Serikari ingekuwa inaamini ushirikina, ningemrudisha mwanangu Kanumba, maana najua hajafa, bali amechukuliwa msukule…” hivyo ndivyo alivyoanza kuzungumza Flora Mtegoa au Mama Kanumba ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita aliamua kutoboa siri nzito ya moyoni mwake, Mama Kanumba aliyaongea hayo nyumbani kwa marehemu, maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa mama huyo kufunguka kwa undani ikiwa ni siku 23 tangu afariki mwanaye Kanumba na kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.

Mama Kanumba akiwa nyumbani  alimpigia simu mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Ayubu akidai ni ndugu wa marehemu kwa upande wa baba mzazi, Mzee Charles Kusekwa.
Kwa wakati huo, Ayubu alikuwa Shinyanga akamuunganisha na mwanahabari wetu.
 Akianika kila kitu kwenye simu, Ayubu alianza kwa kudai Baba Kanumba ni kigeugeu kwa familia huku akijua mila za Kisukuma haziendani na matakwa yake.
“Unajua ndugu mwandishi namshangaa anko (Baba Kanumba), anawezaje kugombea mali za marehemu wakati hakumtolea mahali Mama Kanumba? Hii mila amejitungia mwenyewe, Kisukuma hatakiwi  kuuliza mali maana hakumtolea mahali mama wa marehemu,” alisema Ayubu.
 Katika mwendelezo wa mazungumzo hayo, ndipo mazito nyuma ya pazia yakaibuka kwani Mama Kanumba aliweka wazi kuwa kwa sasa mali za marehemu zinamfanya atishiwe maisha na Baba Kanumba.
Aidha, mama huyo wa marehemu alifika mahali akasema kuwa amekuwa akipokea simu za vitisho ambazo zinamtaka akumbuke alipo mwanaye, hivyo akifanya mchezo na yeye atamfuata huko lakini kisa kikubwa kikitajwa kuwa ni mali za marehemu Kanumba.
Mama Kanumba akatoa wito: “Watanzania niombeeni sana, maana natishiwa maisha sasa, naulizwa kama najua alipo mwanangu, nikifanya mchezo na  mimi nitakwenda huko.”
   Akizidi kuweka wazi siri nzito, mama huyo wa marehemu alisema mwanaye alijulishwa juu ya kifo chake.
Alisema mtu aliyedaiwa kumpa tahadhari hiyo ni ndugu wa karibu wa Kanumba (jina halikutajwa) akiambiwa kuwa kuna mganga wa kienyeji Shinyanga (jina linahifadhiwa) anatumiwa kuuondoa uhai wake.
Hata hivyo, alisema marehemu alikuwa akidharau kwa vile hakuwa akiamini ushirikina ingawa siku zilivyozidi kukatika, aliamua kuita watumishi wa Mungu na kufanya misa nyumbani kwake, Sinza.
“Kanumba alionywa na ndugu yake mmoja, akamwambia huku Shinyanga si kwema kwako, kuna tetesi kwamba yupo mtu anakuwinda kukutoa roho. Hakikisha unasali sana Mungu akusaidie,” alisema mama Kanumba akimkariri ndugu huyo.
Akaendelea: “Alipuuzia kwa sababu hakuwa mshirikina, lakini kuna siku alifanya misa nyumbani kwake ili Mungu amsaidie kumlinda na shetani huyo na siku chache mbele ndiyo akafariki dunia.”

Katika kile kinachodaiwa kuwa Kanumba amechukuliwa msukule, tamko linalotoka na mama na kaka wa marehemu ni kwamba mganga mmoja mashuhuri mjini Shinyanga anadaiwa kufika katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kufanya kafara ya kumwondoa Kanumba.
“Unajua tuliambiwa kuwa huyo mtu aliyekuwa akiisaka roho ya marehemu alimwita mganga huyo ambaye alifika nyumbani wiki tatu kabla ya kifo cha Kanumba  na kufanya makafara yaliyokuwa na damu na jina la Kanumba.
“Aliyetuambia mchezo mzima alidai kuwa katika kufanya kafara hilo, mganga alichukua damu na kuchora jina la Kanumba huku akisema kuwa haitachukua siku, ataaga dunia,” alisema Mama Kanumba.

Mama Kanumba aliendelea kuweka wazi kwamba kifo cha mwanaye kilitokea yeye akiwa Bukoba, alipotua Dar kabla ya mazishi, kuna mtu alimpasha habari za kutisha kuwa Kanumba hajafa, kachukuliwa msukule.
Akasema: “Ilibidi Jumatatu (Aprili 9, 2012) tutume wanandugu kwenda Kanisa la Efatha kwa Mchungaji na Nabii Josephat Mwingira kwa ajili ya maombi ya kumrudisha marehemu baada ya kuambiwa alichukuliwa msukule.”
“Mwanangu (mwandishi) ulishawahi kusikia misukule inarudi? Ndicho kilichotokea, hakurudi hata baada ya maombi yale.”

Siri ziliendelea kuvuja, mwanafamilia mmoja naye akasema kuwa pamoja na umati kujitokeza kwenye Viwanja vya  Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu, hawakufanikiwa kufanya hivyo kwa sababu za kishirikina.
“Kwa kweli kilichotokea pale kwa watu wanaojua ushirikina unavyofanya kazi wataamini, yule mganga aliyemmaliza Kanumba alifanya kila njia, watu wakawa wanakanyagana, utaratibu ukafa, kwani angeruhusu watu wote kuaga kuna wengine wenye macho ya kiroho, wengine kichawi wangegundua Kanumba wa kwenye jeneza si binadamu,” alisema mwanafamilia huyo (jina linahifadhiwa).

Hili nalo ni jipya, kwani kwa mujibu wa Mama Kanumba, baada ya kuambiwa mwanaye alichukuliwa msukule, familia iliamua kumzika sanjari na Biblia pembeni ili mwili wake usiondolewe kaburini na hao waliomchukua msukule.

Alipotafutwa Baba Kanumba ili azungumzie tuhuma zilizopo za kutoa vitisho, aliomba kupigiwa baadaye kisha akakata simu.

Habari tulizozipata wakati tunakwenda mtamboni zinadai kuwa Jumamosi, familia ya Mzee Kanumba iliyopo Shinyanga ilikaa kikao kizito cha kumteua msimamizi wa mirathi ya mali za marehemu Kanumba.

U-FREEMASON WA KANUMBA HUU HAPA

MENGI yamesemwa na yanaendelea kusemwa kwamba, mpaka kifo chake, Marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ alikuwa mwanachama wa imani ya Freemason (wajenzi huru) ambayo inashika kasi katika nchi za Kiafrika, lakini mama wa marehemu, Flora Mtegoa ametoa tamko juu ya tuhuma hizo za mwanaye.
Akizungumza na waandishi wetu hivi karibuni nyumbani kwa marehemu Kanumba, maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar, mama Kanumba alisema amesikia kuwa mwanaye alikuwa muumini wa imani hiyo yenye utata duniani.
Lakini akasema: “Namjua Kanumba, alikuwa mwanangu, mambo yake mengi nilikuwa nayajua maana tulikuwa tunaishi kama marafiki, habari hizo si za kweli.
“Watu wanasema sana, sijui wanatumia vigezo gani? Mwanangu alikuwa muumini mzuri sana wa Kanisa la African Inland Church (AIC), sasa huo u-Freemason aliuchukulia wapi?”
http://fc01.deviantart.net/fs70/f/2010/181/5/7/devil__s_kingdom_cardgame_by_paulobarrios.jpg

Akizidi kumimina maneno kwenye kalamu za waandishi wetu, mama Kanumba alisema kuwa kama ni suala la picha ambazo watu wanasema alipiga akiwa na mapozi ya imani hiyo, ni kwa kutokujua lakini si kweli kwamba alikuwa muumini wa jamii hiyo.
“Huo ni uzushi uliopitiliza,” alisema mama Kanumba.

Wengi mitaani wamekuwa wakisema baadhi ya picha za marehemu Kanumba zilionesha viashiria vya kuwa mfuasi wa imani hiyo ambayo mpaka sasa Watanzania wengi hawaijui vizuri.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7jzxZ1q6AN2Xk_2oSxu6k43vc0ZKTziydPkH_o9lF6BbxqNFBjIbE9dwUiu1b_sB4KEseNmdXuu8E5cqmy6aD8Yei_fwaqQDyy2EQP3BMcL1P5WAJ37rshKM-OfSCxOZGX8pGOmYTQEk/s400/dev1.gif
Zipo baadhi ya picha ambazo marehemu Kanumba anaonekana akiashiria alama za Freemason. Mfano, kuna picha ambayo mkono wake wa kulia ameweka vidole mfano wa pembe za mbuzi.
Aidha, kuna picha marehemu amevaa tisheti nyeusi yenye picha kubwa ya fuvu la binadamu linalodaiwa kuwa miongoni mwa nembo za Freemason. Picha nyingine marehemu amevaa cheni yenye kidani ambacho kinasadikiwa ni utambulisho wa u-Freemason.

Miongoni mwa magumzo yaliyotikisa siku ya kuuaga mwili wake ni suti nyeusi aliyovalishwa ambapo upande wa kushoto wa koti kuna nembo inayotafsiriwa ni ya Freemason.

Waandishi wetu waliwasiliana na mama wa marehemu na kumuuliza nani aliyemvisha koti hilo, yeye alijibu kwa kifupi:
“Sijui ni nani?”

Kigezo kingine ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakikiamini kwamba marehemu alikuwa muumini wa dini hiyo ni kasi ya mafanikio yake.
http://www.artsparkdesign.com/wp-content/uploads/2012/02/itstimelogo.jpgWengi wanasema kuwa marehemu Kanumba alikuwa mcheza filamu kama wengine, wakiwatolea mfano akina JB, Rich, Frank, Pastor Muyamba, Claud, Dk. Cheni na wengineo, lakini yeye kasi ya maendeleo ilikuwa kubwa zaidi ukilinganisha nao.
Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu wakasema kuwa wamesikia mtu anapokuwa Freemason anawezeshwa kwenye shughuli zake kwa kuwa na bahati ya kutajirika.
 
 Baadhi ya watu wamekuwa wakitaja mvuto aliokuwa nao marehemu kwamba nao ni dalili tosha kuwa alikuwa kwenye imani hiyo.
Wengi waliodai wana elimu kuhusu Freemason walisema kuwa, mara nyingi mwanachama wao hupoteza maisha wakati nyota yake ikiwa inawaka sana.
Walitoa mfano wa marehemu Pepe Kalle, kwamba alipotoa albamu ya Cocktail aliwika sana na ndipo alipoaga dunia ghafla.

Bado wengi wanazidi kuamini kifo cha ghafla cha Kanumba kinafanana na cha maarufu wengine duniani, marehemu Michael Jackson ‘The Jacko’, Whitney Houston na Madilu System ambao pia walihusishwa na u-Freemason.

Watu hao wanaopepeta huko mitaani kuwa marehemu Kanumba alikuwa muumini wa imani hiyo walizidi kuibua mapya ambapo wanaamini nyota wa filamu za Nollywood (Nigeria), Ramsey Noah naye ni mwanachama wa dini hiyo.
Wakadai mcheza filamu huyo alikuja Bongo na kucheza na Kanumba Filamu ya Devil’s Kingdom ambayo sehemu kubwa ya stori ni maisha ya imani ya Freemason.

“Mimi nina wasiwasi na Noah (Ramsey), yule jamaa nasikiasikia naye ni muumini, sasa alikuja hapa kwetu (Tanzania) akacheza na marehemu filamu ya Devil’s Kingdom, huenda alimuingiza mwenzake kwenye imani hii,” alisema Rukia, mkazi wa Ubungo Kibangu jijini Dar.
Ili kunogesha habari hizo, ilidaiwa kuwa baadhi ya waigizaji wa filamu hiyo akiwemo Ramsey mwenyewe walipatwa na masahibu ambapo ukiacha Kanumba aliyefariki, staa huyo wa Nigeria alipata ajali huku Kajala Masanja akisota Segerea hivyo inawezekana walibumburua siri za Freemason kupitia Devil’s Kingdom, jambo ambalo waumini wa imani hiyo hawakulipenda.